Serikali imesema kuwa ahadi iliyotolewa na Rais Magufuli ya kuaajiriwa vijana 2500 walioshiriki katika ujenzi wa ukuta wa Mererani waajiriwe zoezi hilo limeanza.
Akizungumza leo Bungeni jijini Dodoma, Mei 31 2018,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akijibu swali la Mbunge Machano aliyehoji,
Wakati wa uzinduzi wa Ukuta wa Mererani ambao Mh. Rais alizindua, Rais alifurahishwa na kazi iliyofanywa na Jeshi na aliahidi vijana 2500 wa JKT ambao waishiriki katika ujenzi huo waajiriwe na vyombo vya ulinzi vya Tanzania , Je ni hatua gani imefikia kuhusu ajira zao mpaka sasa?
“Ni kweli kwamba Mh. Rais alitoa ahadi kwa vijana walioshughulika katika ukuta pale Mererani, na zoezi hilo kwa kweli lishaanza Polisi wamepokea vibali vya ajira usahili umeanza nimategemeo yetu vyombo vingine vya ulinzi na usalama watakapo kuwa wamepata vibali wataanza kuwachukua vijana hawa,” amesema Dkt. Mwinyi.

Huu ndio ukuta uliojengwa na vijana hao
Ukuta huo ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, April 6 mwaka huu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: