Monday, 4 June 2018

Singida United na KMC zaliliwa kumdhalilisha kocha


Baada ya klabu ya soka ya Kinondoni Municipal Council FC kumchukua kocha Ettiene Ndayiragije na kumtema kocha aliyeipandisha ligi kuu Felix Minziro, kocha huyo amelalamika kutotendewa haki na kudhalilishwa.
Minziroa ambaye pia aliipandisha Singida United kisha kuachwa na kuchukuliwa kocha Hans Van Pulijm amesema ameshangazwa na uamuzi uliochukuliwa na Manispaa hiyo na kuongeza kuwa walichokifanya ni sawa na kumdhalilisha.
"Hawajanitendea haki, waliniita siku moja kabla na kunieleza kuwa wanaachana na mimi lakini ndani ya muda mfupi wakamtangaza kocha mpya, maana yake walikuwa na mipango chini chini na huo ni nudhalilishaji kwa kocha laiyetumia nguvu nyingi kuipandisha timu'', amesema.
Kuondolewa kwa Minziro kwenye benchi la ufundi la KMC inamfanya sasa ajiwekee rekodi ya kuwa kocha aliyepandisha timu kwa misimu miwili mfululizo kisha kufukuzwa kazi na timu hizo.
Mbali na KMC timu nyingine ambazo zimepanda kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao ni pamoja na JKT Tanzania, African Lyon zote za Dar es salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance FC ya Mwanza na Biashara United ya Mara.

No comments:

Post a Comment