Saturday, 2 June 2018

Rais Magufuli awapandisha vyeo Maafisa 9 wa Magereza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 4 wa Jeshi la Magereza kutoka Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP) hadi kuwa Kamishna wa Magereza (Commissioner of Prisons – CP).

Pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Magereza wengine 5 kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (Senior Assistant Commissioner of Prisons – SACP) hadi kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP).

Maafisa waliopandishwa vyeo kutoka DCP na kuwa CP ni wafuatao
  •    Hamis Ngarama
  •     Tusekile Mwaisabila
  •     Augustine Sangalali Mboje
  •     Gideon Marco Nkana
Maafisa waliopandishwa vyeo kutoka SACP na kuwa DCP ni,
  •    Julius Mayenga Sang’udi
  •     Afwilile Mwakijungu
  •     John William Masunga
  •     Phaustine Marint Kasike
  •     Joram Yoram Katungi

No comments:

Post a comment