Monday, 4 June 2018

Kutinyu Atambulishwa Rasmi Azam FC

Na Hezbon Mahaulane
Uongozi wa klabu ya Azam FC umeamua kumtambulisha rasmi aliyekuwa mchezaji wa Singida United, Tafadzwa Kutinyu katika kikosi chao.
 
Kutinyu ameingia mkataba wa miaka miwili na Azam ambapo ataingia kambini kuanzia Julai 3 2018 kuanza rasmi maandalizi ya msimu ujao wa ligi zitakazoanza kuchezwa.
 
Mzimbabwe huyo alijunga na Singida United akitokea klabu ya Chicken Inn inayoshiriki ligi kuu Zimbambwe. 

Kutinyu amesaini Azam, usajili unaoelezwa umegharimu kiasi cha dola 2 0,000 kwa Singida kumuachia.

No comments:

Post a comment