# Halmashauri yatakiwa kuweka alama za vibao kwenye maeneo yote mipaka  ya halmashauri ikionesha kuingia na kutoka katika halmashauri hiyo.
# Kuweka mikakati thabiti ya kujenga mabweni ya wanafunzi kwenye shule za sekondari zote huku kipaumbele kikiwa kwaenye shule zilizo maeneneo ya pembezoni na kumalizia majengo ambayo tayari yameanza.
# Halmashauri  kuandaa maandiko ya miradi ya kimkakati kwa ajili ya kuwekeza kwenye eneo la Burka, ikiwa ni miradi ambayo serikali ya awamu ya tano inaipa kipaumbele ili kuzijengea uweo halmashauri kujipatia mapato.
# Watalamu wametakiwa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi bila kujali tofauti za kisiasa, kidini, kwa kusimamia maono ya halmashauri hiyo ya kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo.
# Licha ya Halmashauri kufanikiwa kutekeleza miradi mingi ya Maendeleo, kwa robo ya tatu, lakini pia watalamu wametakiwa kuhakikisha kipindi cha robo ijayo ya mwisho, halmashauri inafikia malengo yaliyopangwa kwenye bajeti.
# Aidha kuongeza bidii ya ukusanyaji mapato kufikia asilimia 37% zilizosalia kukamilisha mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 na kuweza kufikia malengo.
# Halmashauri imefanya vizuri katika utoaji wa mikopo ya wanawake na vijana kwa kutumia asilimia 10%ya mapato ya ndani, licha ya changamoto ya baadhi ya wananchi kulalamikia kutokupata mikopo hiyo na kuitaka Idara ya Maendeleo ya Jamii kuendelea kuelimisha jamii juu ya uundaji wa vikundi na utoaji wa mikopo.
# Miradi miwili ya maji ya  Ngaramtoni na Loovilikuny, moja ya miradi ya vijiji kumi, imeshakamika kwa asilimia zaidi ya 98%  Halmasmashauri ifanye juhudi za kuhakikisha inakabidhiwa ili wananchi waweze kupata huduma ya hiyo ya maji ambayo ambayo waimeisubiri kwa muda mrefu sasa ili kuwaondolea kero kwa wananchi wa maeneo hayo.
# Wakala la Barabara mijini na vijijini (TARURA),  kuendelea kubainu uharibifu wa miundombinu ya barabara zote za halmashauri zilizoharibiwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ili kuweka mikakati ya ukarabati wa barabara hizo mara baada ya kumalizika kwa msimu wa mvua.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: