Friday, 4 May 2018

Wizara ya Elimu yakanusha Kitabu kinachosambaa Mitandaoni


TAARIFA KWA UMMA

Kumekuwa na taarifa za makosa ya vitabu inayozagaa  mitandaoni ikionyesha picha inayoelezea viungo vya mwili wa binadamu.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kuutarifu Umma kuwa kitabu kinachosambazwa si chapisho la Taasisi ya Elimu Tanzania - TET, na wala si miongoni mwa vitabu ambavyo vimesambazwa kwenye shule.

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Pia kitabu kinachosambazwa Hakina uhusiano wowote na wala hakifanani na vitabu ambavyo vimechapishwa  hivi karibuni na TET.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawasihi Watanzania kupuuza taarifa hizo zenye nia ya kupotosha.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
4/05/2017

No comments:

Post a Comment