Wananchi wamelalamikia baadhi ya wajumbe wa mitaa wanaowapokea wageni bila kuwatolea taarifa za msingi nakupelekea ongezeko la wizi katika mitaa mbalimbali ikiwemo mtaa wa bugosi wilayani tarime

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi  katika mkutano wa maendeleo ya mtaa wa bugosi  wakati wakitoa kero za mtaa huo ambapo wamedai kuwa baadhi ya wajumbe wamekuwa wakiishi na wezi katika maeneo yao ikiwemo baadhi ya wezi hao kukamatwa na Mali za wananchi hao ikiwemo pikipiki

Aidha Mjumbe wa mtaa wa robi mwita werema ambaye ametuhumiwa kuishi na wapangaji wanaoshiriki na kusababisha wizi katika mtaa huo amesema kuwa watuhumiwa hao aliwapokea katika mtaa wake na kuwapatia Nyumba ya kuishi pasipo kujua tabia  zao nakuhaidi kutoa ushirikiano katika kuhakikisha wanakomesha wizi katika eneo hilo

Aidha mwenyekiti wa mtaa wa bugosi Zakaria ametoa wito  kwa wajumbe wote  kuhakikisha wanapata taarifa rasmi za mwananchi anayehamia mtaani kwake ili kuondoa changamoto ya wizi katika maeneo yao

Naye polisi jamii katika kata ya nyamisangura Paulo Stivini Moshi amewaomba  kutoa ushirikiano pindi wanapobaini jambo hilo ili kupunguza wizi huo nakuwataka akina mama wanaojihusisha na uuzaji wa vilevi kutouza pombe muda wa kazi
Share To:

msumbanews

Post A Comment: