Thursday, 24 May 2018

Wananchi wote wenye viwanja vilivyopimwa halmashauri ya Arusha wanatakiwa kulipa Kodi ya Ardhi kabla ya tarehe 30.05.2018


Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, anawatangazia wananchi wote wenye viwanja vilivyopimwa ndani ya mipaka ya halmashauri hiyo, kulipa Kodi ya Ardhi kabla ya tarehe 30.05.2018.

Kadhalika wamiliki wote wa viwanja katika eneo la Endurace (Kivulini ) lilipokuwa shamba namba 181/3/2  wanatakiwa kufika ofisi za Ardhi chumba Na. 3  ili kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 30/05/2018, kutokulipa kodi kutasababisha kupelekwa Mahakamani na viwanja vyao kuuzwa.

Kwa wale wote waliotumiwa Hati ya Madai (Demand Notes ) wanatakiwa kulipa kabla ya  tarehe hiyo, endapo tarehe hito itapita watapelekwa Mahakamani.

No comments:

Post a comment