Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala cha robo ya tatu kimeendelea leo kwa kamati tatu za fedha, uchumi na mipango miji zikisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha Januari  na Machi Mwaka huu.

Akisoma taarifa ya kudumu ya kamati ya uchumi na huduma za jamii Kaimu Mwenyekiti, Helen Lyatula amesema kamati yake imesimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali mbalimbali za miradi ya maendeleo ikiwemo kusimamia taaluma na nidhamu katika shule zote za awali na msingi za Serikali na zisizo za Serikali na kutoa muongozo na utaratibu mbalimbali wa kufanikisha malengo waliyoweka kulingana na sera ya elimu.

" Jumla ya walimu 1653 wa shule ya msingi wanatarajia kupandishwa vyeo na madaraja, lakini halmashauri pia imepokea vitabu 100, 904 toka TAMISEMI na kusambaza kwa shule zote msingi," amesema Lyatula.

Alisema pamoja na mafanikio waliyoyapata bado kumekuwepo na changamoto zinazokabili idara na vitengo katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa madai ya likizo hadi sasa jumla ya walimu wa shule za msingi 1837 wanadai kiasi cha Tsh 478,346,684,00, pamoja na ukomo wa bajeti katika utekelezaji shughuli mbalimbali za kilimo, ushirika na umwagiliaji.


Taarifa ya kamati ya fedha na utawala yenyewe imesimamia mapato na matumizi ya Halmashauri ambapo imekusanya jumla ya Tsh 10,348,333,506 sawa na asilimia 88 ya makisio ya Tsh 11,793,447,388.50 bila kuweka kodi ya majengo ya Tsh 800,000,000.00 ambazo zinakusanywa na Serikali kuu kutoka vyanzo vya ndani ya Halmashauri.

Akisoma taarifa hiyo Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Waziri Mweneviale amesema katika kipindi cha robo hii, halmashauri imefanikiwa kushinda kesi takribani saba ikiwemo kesi na. 54/2003 kati ya Charles Moses dhidi ya halmashauri ya manispaa hiyo ambapo mdai alikuwa akiidai halmashauri kiasi cha Tsh 1,500,000,000 hivyo kwa kpindi hiki kamati imeokoa kiasi hicho cha fedha.

Aidha kamati hiyo iliidhinisha matumizi ya force account kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa pavement katika hospitali ya Mama na Mtoto Chanika kwa gharama ya Tz 183,864,091.20 .
Share To:

Anonymous

Post A Comment: