Thursday, 17 May 2018

UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA KUKAMILIKA MWEZI JUNI

Na. Theresia Mwami - TEMESA

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), imeahidi kukamilika kwa ujenzi kivuko kipya cha Kigongo Busisi (MV. MWANZA) unaofanywa kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ifikapo mwezi Juni 2018. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria 1,000 kwa wakati mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa kivuko hicho, uliofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA mapema leo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu alisema ujenzi huo unagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 8.9 na ulianza rasmi tarehe 28/08/2017 na kwamba tayari umekamilika kwa asilimia 95.

“Namuagiza Mkandarasi kuhakikisha kuwa ujenzi wa kivuko hiki unakamilika kwa aslimia 100 ifikapo mwezi Juni,2018 kama ilivyoainishwa kwenye mkataba ili kuweza kuboresha zaidi huduma ya uvushaji abiria na mizigo yao katika eneo Kigongo – Busisi”, aliongeza Dkt. Mgwatu.

Aliongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kivuko cha MV. MWANZA kutafanya eneo la Kigongo Busisi kuboresha zaidi huduma za uvushaji kwani kwa sasa tayari kuna Kivuko cha MV. Misungwi ambacho pia kina tani 250, MV. Sengerema tani 170 na MV. Sabasaba tani 85.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TEMESA Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri alisema kuwa, serikali inalengo la kuboresha hali ya maisha ya wananchi, kwa kuwawekea miundombinu salama ya vivuko, ili kuhakikisha wanapata huduma bora na salama wakati wote. 

Aliongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutatoa nafasi ya ukarabati mkubwa wa vivuko vingine vinavyotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi kufanyika kwa awamu. Aidha alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza TEMESA kwa kazi nzuri ya usimamizi wa ujenzi wa kivuko hicho, kwa kuhakikisha kuwa unakamilika kwa wakati kama ilivyo kwenye mkataba wa ujenzi wake.

1Nae Mkurugenzi Kampuni ya Songoro Marine Transaport Boat Yard Ltd, Major Songoro, aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuiamini kampuni hiyo na kuahidi kuimaliza kazi hiyo kwa haraka na ustadi mkubwa.
Kivuko kipya cha MV. MWANZA chenye uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria 1,000 kwa wakati mmoja, kinachojengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ambacho kinagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 8.9 fedha kutoka serikali ya Tanzania. Kitatoa huduma kati kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.
2
Kivuko kipya cha MV. MWANZA chenye uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria 1,000 kwa wakati mmoja, kinachojengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ambacho kinagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 8.9 fedha kutoka serikali ya Tanzania. Kitatoa huduma kati kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.
3
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri, akipanda ngazi kukagua ujenzi wa kivuko kipya cha MV. MWANZA, nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transaport Boat Yard Ltd (inayojenga kivuko hicho) Salehe Songoro, akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme( TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu.
4
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme( TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari baada ya ukaguzi wa kivuko kipya cha MV. MWANZA kulia kwake mwenye miwani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri.Picha na Kitengo cha Habri na Mawasiliano TEMESA

No comments:

Post a comment