Thursday, 10 May 2018

SIMBA WAANZA SAFARI KUELEKEA SINGIDANa George Mganga

Kikosi cha Simba kimeanza safari ya kuelekea Singida kwa ajili ya mtanange wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United.

Simba itapitia katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma, kuweka kambi fupi kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea mjini Singida.

Taarifa kwa mujibu wa Meneja wa kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi, Richard Robert, amesema kuwa kikosi kitapita jijini hapo ili kuweka kambi fupi kabla ya kuendelea na safari.

Inaelezwa kuwa Simba wamepanga kupitia Bungeni kwa ajili ya kupata baraka za kuelekea mechi yao na Singida itakayopigwa Mei 12 kwenye Uwanja wa Namfua.

Tayari kikosi hicho kipo njiani hivi sasa kuelekea jijini humo na kesho kitaanza tena safari ya Singida.

No comments:

Post a Comment