Sunday, 13 May 2018

Ray C: Nikifanya Hivyo Nitapelekwa jela na Rais Magufuli

Muimbaji mwenye sauti aina yake kutoka Bongo, Ray C amesema ukali wa Rais Magufuli umepelekea wasanii waliokuwa na tabia ya kupiga picha za utupu kuacha.

Ray C akiwa nchini Kenya amesema tabia hiyo kipindi cha nyuma ilishamiri ila kwa sasa inaenda ikipungua.

“I don’t know lakini inakuwa too much inaenda inakuwa too much ndio maana Rais Magufuli kakataza, siunajua Baba yetu mkali kidogo. It was too much ilikuwa inaanza kwenda mbali, unajua watoto wanaangalia,” Ray C ameiambia Citizen TV.

Alipoulizwa kwanini yeye hafanyi hivyo alijibu; “Sinitapelekwa jela na Rais Magufuli, yeah!, is not allowed,”.

Mapema January mwaka huu Serikali ilimuita msanii Gigy Money na Mwanamitindo Sanchoka kwa mahojiano maalumu kuhusu kazi zao ambazo zilionekana zipo kinyume na maadili hususani kwenye mavazi wanayovaa.

No comments:

Post a comment