Tuesday, 1 May 2018

Rais Magufuli akataa ombi la nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekataa ombi la kuongeza mshahara kwa wafanyakazi iliyoombwa na TUCTA.
Akizungumza leo Mei 1 mkoa Iringa katika siku ya Wafanyakazi amesema kuwa kwasasa fedha nyingi zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maendeleo.
“Kwangu mimi ninafikiria hizi pesa tunazotoa kwa ajili ya elimu bure ni nzuri kuliko fedha hizo kuzipeleka kuongezea mishahara, naona bora kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu kuliko kuongezea wafanyakazi mishahara,” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa Mwaka huu wataendelea kutoa nyongeza ya kawaida ya mishahara ya mwaka na wanataka wafanyakazi wote wapate stahiki zao.

No comments:

Post a Comment