Friday, 11 May 2018

Mombasa nina nyumba tayari – Alikiba

Msanii wa muziki kutoka RockStar4000, Alikiba amethibitisha kuwa na nyumba yake ya kuishi Mombasa nchini Kenya.
Muimbaji huyo ambaye amezindua kinywaji chake cha Mofaya siku ya sherehe ya harusi yake, amesema kwa sasa akienda Mombasa nafikia nyumbani kwake kwani tayari ana nyumba.
“Mombana nina nyumba tayari, sasa hivi nikienda nafikia nyumbani,” Alikiba alikiambia kipindi cha 360 cha Clouds TV baada ya kuulizwa na mtangazaji kama ana mpango wa kujenga nyumba au kununua.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amesema kinywaji chache cha Mofaya kitaingia sokoni rasmi ya siku kuu ya Eid el Fitri mapema mwezi ujao huku akishindwa kuweka wazi bei ya kinywaji hicho.
Alisema kwa sasa wametangaza deal kwa makampuni mbalimbali ambayo yatapenda kuwa mawakala wa kusambaza kinyaji hicho ambazo kimeonekana kuwa muaarufu kwa siku za karibuni.

No comments:

Post a Comment