Friday, 18 May 2018

Mkuu wa Mkoa Morogoro ampa siku 14 Mkandarasi wa Maji


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen ameagiza mkandarasi aliepewa kazi ya kujenga mradi wa maji katika kijiji cha Kibwaya kata ya Mkuyuni kurudi mara moja kufanya marekebisho licha ya mradi kuwa katika kipindi cha matazamio ya kukabidhi.

Baada ya malalamiko hayo ya wananchi kumfikia Dk. Kebwe na kwenda  kujionea amebaini kuwa mradi huo umejengwa chini ya kiwango huku mkandarasi akiwa amepokea fedha zote ametoa msimamo wa Serikali kumtaka mkandarasi kurudi kufanya marekebisho.

"Nampa siku 14 Mkandarasi wa mradi huu hata kama yupo chini ya wizara ya maji, lakini hizi ni kazi za serikali na mimi ndiye Mkuu wa Mkoa. Arudi afanye masahihisho yote. La! sihivyo atafata nyayo kama yule mwenzake aliyetuharibia barabara ya lami kule kilosa, mnajua kitu gani nilimfanya" Dk. Kebwe.

Licha ya maagizo hayo pia mkuu huyo wa mkoa amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa halmashauli ya wilaya ya Morogoro Sudi Mpili kufuatilia kwa karibu marekebisho ya mradi huo sambamba na kumrudisha mhandisi wa maji aliyesimamia mradi huo  Eng. Steven Mkalimoto ambae kwa sasa amehamishiwa wilayani Mbozi.

"Siku 14 kama hatafika kufanya marekebisho atarudi chini ya polisi atasaini asubuhi anakwenda kazini kila siku mpaka kazi ikamilike. Mkurugenzi Hakikisha sehemu zote maji yanapovuja hakikisha anaziba na kwenye tenki kuna ufa arekebishe sehemu zote. Nimepanda kuangalia nimeona maji yanaingi hivyo amalizie marekebisho," Dk. Kebwe

Mradi huo ambao unagharimu zaidi ya shilingi milion 650, ulitakiwa kukamikila tangu mwaka 2015, ukiwa na Tanki moja pamoja na vituo 15 vya kuchotea maji , ambapo kwa sasa upo katika kipindi cha matazamio huku wakazi wa eneo hili wakidai baadhi ya vituo havijawahi kutoa maji.

No comments:

Post a comment