Saturday, 12 May 2018

Kwa Simba hii weka mbali na watoto

Kikosi cha Simba kimefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1 – 0 ugenini dhidi ya Singida United uwanja wa Namfua na kuendeleza ubabe wake wakutokupoteza.
Mabingwa wapya wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Simba wanaifunga Singida United kwa mara ya pili sasa baada ya mchezo wa kwanza uliyopigwa jijini Dar es Salaam kuibuka na ushindi wa mabao 4 – 0.
Mfungaji pekee wa bao la leo la klabu ya Simba ni Shomari Kapombe dakika ya 24 kipindi cha kwanza na hivyo kuwafanya mabingwa hao wapya kutopoteza hata mchezo mmoja mpaka sasa huku wakijikusanyia jumla ya pointi 68.
Kwenye mchezo mwingine uliyopigwa hii leo timu ya Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya Njombe Mji na kufikisha jumla ya pointi 31 wakiwa nafasi ya 10 wakati vijana wa njombe wakiburuza mkia kwakuwa na alama 22 nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi.

No comments:

Post a Comment