Wednesday, 9 May 2018

Kati ya wasanii 5 wenye fedha Bongo Aslay ni wa tatu, Nandy aeleza

Msanii wa muziki Bongo, Nandy amefunguka na kusema kuwa Aslay ni miongoni mwa wasanii wenye fedha nyingi zaidi Bongo.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Ninogeshe’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa Aslay ni miongoni mwa wasanii watano ambao wana fedha zaidi Bongo.
“Katika top five naweza kumuweka kwenye namba tatu, siwezi kutaja wa kwanza wala wa pili ila ni namba tatu,” amesema Nandy.
Ameendelea kwa kusema kuwa baada ya Aslay yeye ndiye anafuata, yaani namba nne kwa kuwa na fedha nyingi. Utakumbuka Aslay na Nandy wameshatoa ngoma mbili pamoja, Mahabuba na Subalkheri.

No comments:

Post a Comment