Johari Amtaka Hamisa Aachane na Diamond - MSUMBA NEWS BLOG

Wednesday, 30 May 2018

Johari Amtaka Hamisa Aachane na Diamond

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amempa somo mrembo Hamisa Mobetto kwa kumtaka aachane na Baba watoto wake Diamond Platnumz.

Johari amefunguka na kudai kuwa ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na staa hivyo anajua ni jinsi gani walivyo pasua kichwa hivyo anamshauri Mobetto aachane na Diamond.
 
Kwenye mahojiano  na Global Publishers, Johari amemtaka  Mobeto, asirudi kwa Diamond, bali angeendelea na maisha mengine maana kurudi ni kuambulia maumivu tu, hakuna cha maana zaidi.

"Ningekuwa nimepata nafasi ya kumshauri Mobeto, ningemwambia asimrudie Diamond, lakini ndiyo hivyo nilisikia wako pamoja tena, ninachoweza kumwambia ni awe makini tu maana penzi na staa linaumiza sana. Kwani ni watu ambao hawatulii, atajikuta anajipotezea muda na baadaye kuja kujuta.

"Nimewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa, uliniumiza sana na ndiyo maana nampa somo Mobeto kuwa makini sana ili kukwepa kuumiza moyo wake na kupoteza muda”.

Johari alishawahi kuwa na uhusiano wa muda mrefu na staa wa Bongo movie Ray Kigosi lakini walikuja kuachana na Ray kuzaa na Chuchu Hansy.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done