Friday, 18 May 2018

HALOTELI YAZINDUA DUKA JIPYA MIKOCHENI SHOPPERS PLAZA


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa mtandao huo wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka hilo.
Baadhi ya wateja waliofika kwenye duka hilo kupata huduma mbalimbali.

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imezindua duka eneo la Mikocheni Shoppers Plaza jijini Dar es Salaam ambapo huduma mbalimbali za mtandao huo zitakuwa zikipatikana.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel , Mhina Semwenda amesema kuwa wateja watakuwa na uwezo wa kujipatia huduma mbalimbali kutoka kwa wahudumu wa duka hilo ikiwemo kuunganishiwa kifurushi kisichokuwa na kikomo cha muda wa maongezi kinachowawezesha wateja wa mtandao huo kufanya mawasiliano bila kikomo, kilichopewa jina la  Super Halo.

Alisema pia wameamua kuwasogezea wateja hasa wa Wilaya ya Kinondoni na maeneo mengine huduma bora jirani na mahali walipo.

No comments:

Post a comment