Sunday, 13 May 2018

Haji Manara awachokonoa wachezaji na mashabiki wa Yanga

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amewakaribisha wachezaji na mashabiki wa Yanga kwenye sherehe za kukabidhiwa ubingwa wa Ligi wa klabu yake ya Simba.
Picha inayohusiana
Haji Manara
Manara amesema hayo jana Mei 12, 2018 mapema baada ya kumalizika kwa pambano kati ya Singida United na Simba SC, mchezo ambao Simba waliibuka kwa ushindi wa goli 1-0 .
Tutawakaribisha wasiwe na wasiwasi hawa ni ndugu zetu, sisi sio wachoyo wa fadhila tutawakaribisha kwenye party zote.“amesema Manara.
Manara amesema klabu yake itacheza mchezo wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar tarehe 30, Mei na watafanya sherehe kubwa kuliko hata  zile za Simba Day.

No comments:

Post a comment