Geoffrey Lea akiwa ameshika mkataba wake wa kurejea tena Clouds FM. Aliyeinama ni Meneja wa Vipindi wa kituo hicho, Shafii Dauda

 Mchambuzi wa soka mashuhuri nchini Geoffrey Lea, amerejea tena kwenye kituo chake cha awali, Clouds FM. 

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

  Geoffrey anajiunga tena na redio hiyo akitokea Azam TV ambapo alikuwa akifanya kazi za uchambuzi wa soka ikiwemo ligi kuu ya Tanzania Bara. 

Clouds wamethibitisha hilo kwenye mtandao wao wa Instagram, kwa kuandika, “#Breaking Usajili Mpya!

Kandarasi mpya ya mtangazaji @geoff_lea kuitumikia #CloudsMediaGroup karibu tena nyumbani Geofrey Lea tulichambue soka.”

Mtangazaji huyo anatarajiwa kurejea tena kwenye kipindi chake cha kuchambua michezo cha Sports Extra.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: