Monday, 14 May 2018

Benki Kuu yaagiza mamilioni ya Dola


Benki kuu ya Zimbabwe imeagiza karibu dola milioni 400 pesa taslimu katika kipindi cha miezi minne iliyopita kufuatia uhaba wa pesa nchini humo.

Gavana wa wa Benki Kuu, John Mangudya, amesema foleni kwenye mabenki zinatarajiwa kupungua katika kipindi cha miezi miwili ijayo huku mapato ya kitaifa yakitarajiwa kuimarika kutokana na mauzo ya tumbaku na dhahabu.

Zimbabwe imekuwa ikikumbwa na uhaba wa pesa tangu mwaka wa 2016 ikichangiwa na gharama ya juu za uendeshaji wa serikali.

No comments:

Post a Comment