Thursday, 24 May 2018

Azam FC waingia Kambini kwa kazi maalum


Kikosi cha Azam FC jana kimeingia kambi maalum kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga na Azam zote zinapigania nafasi ya pili ikiwa ni baada ya kuukosa ubingwa msimu huu uliochukuliwa na Simba.

Ofisa wa Habari wa kikosi cha Azam FC, Jaffer Idd Maganga, amesema kuwa wameingia kambi ili kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mechi hiyo itakayowasaidia kubaki kwenye nafasi ya pili.

Maganga ameeleza wanahitaji nafasi ya Umakamu Bingwa ingawa wamelikosa taji hilo ili kuweka heshima ya klabu kwa kuwa mshindi namba mbili.

Msimamo wa ligi unaonesha Yanga ina alama 51 hivyo inahitaji kushinda mechi zake mbili zilizosalia ili kukamata nafasi ya pili tofauti na Azam ambayo inahitaji sare dhidi ya Yanga kusalia kwenye nafasi yake.

Ijumaa ya kesho Yanga itakuwa inakipiga na Ruvu Shooting wakati Azam wakizidi kufanya maandalizi ya kupambana na mabingwa hao wa ligi kwa msimu wa 2016/17.

No comments:

Post a comment