Askofu Mkuu Mteule wa Kanisa la Anglikana nchini, Askofu Maimbo Mndolwa amesema wao kama Kanisa wana jukumu kubwa la kumuombea Rais Dkt. John Magufuli kwani kazi anazozifanya bila kupewa maombi ni sawa sawa na bure.

 Askofu Maimbo ametoa kauli hiyo leo Mei 21, 2018 muda mchache alipomaliza kufanya mazungumzo ya faragha na Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kusema wanaiona Tanzania inavyoelekea katika neema ya kipekee licha ya changamoto zilizopo.

"Kuna mambo mengi mema yanafanyika changamoto zipo. Changamoto zikiwepo zinakuonesha neema ya kuwepo, sisi tunamuombea Rais Magufuli kwasababu kazi anayofanya bila ya maombi ni bure kwa hiyo kazi yetu kama Kanisa kwanza ni kuomba naye, kumsimika na kumsimamisha lakini pia na kumshauri yale ambayo yanapaswa kushauriana hasa katika maeneo ya changamoto", amesema Askofu Maimbo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu Mteule wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Maimbo Mndolwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: