Tuesday, 29 May 2018

Askari Polisi wawili na raia watatu wauawa katika shambulizi

Askari wawili  na raia watatu wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu mmoja aliekuwa na silaha  mjini Liege nchini Ubelgiji.

Mshambuliaji alikimbilia katika shule moja na  kumteka mwanamke mmoja. Polisi imefaulu kumdhibiti  mtu huyo aliendesha shambulizi hilo.  Polisi wengine wawili wameripotiwa kujeruhiwa katika tukio hilo.

Taarifa nyingine inaarifu kuwa mtu huyo aliendesha shambulizi ameuawa na jeshi la Polisi.

No comments:

Post a comment