Wednesday, 16 May 2018

Akutwa amefariki Mtoni Tarime


Na Clonel  Mwegendao
Mtu Mmoja ambaye hajafahamika kwa Jina wala Sura amekutwa amefariki na Mwili wake ukiwa katika bonde la Mto   Nyabirundu uliopo kitongoji cha  Nyabichune Kijiji Nyabichune kata ya Regicheri Wilayani Tarime Makoani Mara.

Shuhuda wa kwanza katika tukio hilo amesema kuwa majira ya asbuhi jana  alipoenda kuchimba Mchanga Maeneo hayo aliona Mwili huo wa Marehemu na kukimbia kutoa taarifa kwa Viongozi wa Vitongoji na vijiji.

Elias Mbusiro ni Mwenyekiti wa Kitongoji alichokutwa Marehemu huyo pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha NyabichuneFrancis Mwikwabe wanazungumzia Juu ya tukio hilo wakizungumzia tukio hilo wamesema kuwa baada ya kupata taarifa hizo wamepiga simu kwa viongozi ngazi za juu ili kufika eneo la tukio.

“Huyu marehemu anaonekana Mzee lakini bado sura yake hatujaitambua katika kijiji chetu” alisema Mbusiro.

Meshaki Osward  ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Regesheri amedhibitisha uwepo wa Tukio hilo huku akitoa Mwito kwa jamii kujitokeza ili kutambua Mwili huo.

“Polisi tayari wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kuchukua Mwili huo kaam sisi viongozi mpaka saha hatujautambua kama kuna mtu yeyote amepoteza Ndugu yake apige simu Polisi Sirari au Kwa Viongozi wa Vijiji na Kata tukio lililopotokea” alisema Meshaki.

No comments:

Post a comment