Friday, 13 April 2018

Waziri Mwakyembe afanya uteuzi huu

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amemteua Dkt. Joseph Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha Michezo Malya.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, uteuzi huo umetekelezwa kwa mujibu wa sheria ya Na. 9 ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) ya mwaka 1997 ikisomwa pamoja na mwongozo wa uteuzi wa Bodi za Uongozi wa vyuo vya Elimu ya Juu.

No comments:

Post a comment