Wednesday, 11 April 2018

suala la wanafunzi waliopata ujauzito kurudi shule laibuka bungeni


Serikali kupitia Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha imesema kuwa haitarajii kuwarudisha wanafunzi waliopata ujauzito shuleni kwa njia yoyote ile.

Akizungumza leo, Bungeni mjini Dodoma, Nasha amesema kuwa ukiruhusu hilo ni mwanzo wa kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila na sheria zetu haziruhusu ngono katika shule.

“Hata sisi serikali kwa kweli hatupendi kusikia vitendo vya uonevu dhidi ya watoto wa kike, kwasasa mfumo wetu wa elimu umepangwa katika namna ya kuhakikisha wanafunzi wanaopata ujauzito wanapata fursa ya kusoma lakini nje ya mfumo rasmi 

"Kwahiyo kuna fursa nyingine nyingi za kusoma kama nilivyosema katika swali langu la msingi kupitia elimu ya watu wazima lakini vilevile vyuo vya ufundi,“ amesema Nasha.

“Serikali haitarajii na naomba niweke wazi wanafunzi ambao wamepata ujauzito kwa njia yoyote ile hawataruhusiwa kuendelea na masomo  kwasababu ukifanya hivyo  una halalisha na kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila zetu na sheria zetu haziruhusu ngono katika shule za msingi na sekondari.“

No comments:

Post a comment