Monday, 9 April 2018

Serikali Yakiri Magereza Kuzidiwa na Idadii ya Wafungwa


Tanzania inakadiriwa kuwa na wafungwa 40,000 wakati uwezo wa magereza yake ni 30,000 hivyo kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 katika msongamano huo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Hamad Yusufu Masauni wakati akijibu swali la nyongeza la Ruth Mollel ambaye ametaka kujua Serikali inafanya nini kumaliza msongamano wa wafungwa.

Masauni amesema kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 ambapo kwa sasa Serikali inafanya kila namna kumaliza msongamano huo.

Katika swali la msingi Mwantakaje  Haji Juma  (BUBUBU-CCM) amehoji ni lini kituo cha polisi katika jimbo lake kitafanyiwa ukarabati.

Naibu Waziri amesema kituo hicho kitafanyiwa kazi wakati wowote fedha ikipatikana ili kiwawezeshe askari kutoa huduma bora.

No comments:

Post a comment