Mkurugenzi
wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika
hayo Bw. Marcel Katemba akizungumza na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka
Yasiyo ya Kiserikali kutoka katika Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa
Mwanza katika kikao baina yake na Wasajili Wasaidizi hao na wadau wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilicholenga kuboresha namna bora ya
uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
Mkurugenzi
wa Msaidizi Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornald Baraka
akiwakumbusha washiriki mambo muhimu yanayohitaji kuzingatiwa kabla na
baada ya kusajili Shirika Lisilo la Kiserikali kwa wadau kutoka katika
Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza
kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani
humo.
Baadhi
ya wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Mwanza
wakifuatilia mada na mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yakitolea na Msajili
wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza
kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani
humo.
Mmoja
wa mdau kutoka Shirika la Kivulini Bi.Yunice Mayengera akiuliza swali
kuhusu utaratibu wa kuhakikiwa kwa mashirika ambayo awali yalisajiliwa
chini ya Sheria nyingine kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga
kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo kwa kuzingatia Sheria na miongozo
mkoani humo.
Afisa
Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali katika Manispaa ya Ilemela Bw. Yusuph Omolo akitoa
ufafanuzi kuhusu masuala yahusuyo Usajili wa Mashirka Yasiyo ya
Kiserikali kwa wadau wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau
hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo
kwa kuzingatia Sheria na miongozo mkoani humo. Picha na Kitengo cha
Mawasiliano WAMJW.
Na Mwandishi Wetu – Mwanza
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imesema haitasita
kulifutia usajali Shirika lolote lisilo la Kiserikali litakaloenda
kinyume na Sheria na Taratibu za nchi.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Mwanza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali Bw. Marcel Katemba alipokuwa akifungua kikao kati yake na
Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali na Wadau wa
mashirika hayo kwa Mkoa wa Mwanza.
Bw.
Katemba amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya Mwaka 2002 ya
Mashirika Yasito ya Kiserikali inayataka Mashirika hayo kuzingatia
Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Nchi katika utendaji wa kazi zao
kwa mujibu wa Katiba na majukumu yao kiusajili.
Ameongeza
kuwa kikao hicho kimefanyika ili kuwakumbusha wadau wa NGOs kufanyakazi
kwa kuzingatia Sheria za nchi zilizopo kwani baadhi ya mashirika hayo
yamekuwa yakitumika kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria.
“Nawataka
wamiliki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia matakwa ya
usajili wao katika kutekeleza majukumu katika Mashirika yao” alisema
Bw.Katemba
Bw.Katemba
amesema kuwa mpaka sasa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 4,868 ndio
yamehakikiwa na kuyataka Mashirika ambayo hayajahakikiwa yafanye
utaratibu wa kuhakiki kwani mara baada ya kuzinduliwa kwa Tovuti mpya ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Mashirika ambayo hayatakuwa
yamehakikiwa hayataruhusiwa kufanya kazi nchini.
Naye
mdau kutoka Shirika la Baraka Orphanage Bi. Patricia Kamugisha asema
kuwa kikao hicho imewasaidia kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa
hawajafahamu na kuendelea kupata uzoefu utakaowasaidiza kuimarisha
utendaji wa shughuli katika mashirika yao.
“Sisi
kama wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali tunatakiwa kuzingatia
Sheria na Taratibu zilizopo ili tuweze kufanya kazi bila kukinzana na
Sheria” alisisitiza Bi. Patricia.
Post A Comment: