Wednesday, 25 April 2018

Ndege kubwa ya Emirates yamuibua Waziri Kigwangalla ‘Watanzania tumekuwa watu wa hovyo’

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla amechoshwa na baadhi ya watanzania ambao wamekuwa wakikosoa kila kitu hata mambo ambayo ni ya muhimu na yanafaida kwa taifa letu.
Tokeo la picha la Kigwangalla
Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla
Waziri Kigwangalla ameeleza hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya kuonesha furaha yake kufuatia ndege kubwa ya Shirika la ndege la Emirates aina ya Airbus A380 iliyokuwa na abiria 480 kutua kwa dharura katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JKNIA) jijini Dar es salaam.
Kigwangalla aliandika “Emirates A380 just landed in Dar. Unable to land in Mauritius due to bad weather and hence diverted to Dar. 420 passengers need to be accommodated till tomorrow morning. And people said we can’t land an A380 in Dar es Salaam“.
Kufuatia kauli hiyo, wadau wengi wa wametoa maoni yao kwa kumshambulia Kigwamgalla kuwa ndege hiyo haijatua kwa safari za kawaida bali ni kwa dharura na wala sio jambo la kupongeza.
  • prootarimoHahahh.. yaani kuland kwa emergency ndio matambo as if zitatua kila siku!! Mbona hata Ethiopian airway ilitua.
  • salumdogoTunataka itue kila siku sio kwa dharura,Mauritius ni nchi ndogo sana lakini inakwenda huko kwa ratiba sio emergency, shame on you waziri for you post
  • derick_mo@hamisi_kigwangalla Mauritius tuvisiwa tudogo vile linatua dege kubwa kama hilo mara kwa mara, sisi tunashangilia baada ya kuwa limetua JNIA kwa ‘bahati mbaya’? Tukaze buti jamani. Bado tuko mbali mno. Mauritius haina Serengeti, Kilimanjaro wala Ruaha.
  • djmarcmuga@hamisi_kigwangalla Mh, sio uwezo ulivyo mkubwa, ni emergency tunatakiwa sasa tuufanye uwezo uwe mkubwa ili zituwe kila leo zikileta abiria na kuchukua wengine,
Baada ya kusoma maoni hayo, Waziri Kigwangalla amesema kuwa Watanzania wamekuwa watu wa kupinga kila jambo, kwani kitendo cha dege hilo kubwa kutua Tanzania ni faida kubwa kwetu kwani inaitangaza nchi yetu kimataifa.
Watanzania tumekuwa watu wa hovyo sana, yaani hata kitu kizuri chetu tutapinga! Hata fursa kama hii ya kuitangaza nchi yetu kimataifa, Tunapinga.“ameandika Kigwangalla.
Hata hivyo, tayari ndege hiyo imeondoka leo Aprili 25, 2018 asubuhi majira ya saa 2:15 kuelekea katika visiwa vya Mauritania ambapo siku ya jana ilishindwa kutua nchini humo kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.

No comments:

Post a comment