Sunday, 29 April 2018

Mkapa Aitabiria simba kichapo leo


Wakati yakiwa amesalia masaa machache kipute cha watani wa jadi kianze pale Uwanja wa Taifa, mchezaji wa zamani wa Yanga, Kenneth Mkapa, ametoa utabiri wake kuelekea mechi hiyo itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba na Yanga zinakutana leo ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili ya ligi kufuatia ule kwa kwanza timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mkapa amesema kuwa mechi hii huwa si rahisi kutabirika kutokana na upinzani wa aina yake namna unavyokuwa kwa timu hizi mbili.

Akizungumza kupitia Radio EFM kwenye kipindi cha Michezo, Mkapa ameeleza kuwa Yanga inaweza ikapata matokeo leo kutokana na namna wachezaji wa Yanga walivyojipanga.

Beki huyo aliyewahi kuichezea Yanga, amesema Simba wataingia wakiwa wamejiamini kufuatia uzuri wa matokeo waliyonayo msimu huu.

Kutokana na kuonesha kiwango kizuri tangu msimu huu uanze, Mkapa anaamini Yanga watahitaji kuimaliza Simba leo ili ijitengenezee mazingira mazuri pengine inaweza ikautwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo

No comments:

Post a Comment