Friday, 6 April 2018

Mbunge CCM Ahoji Bibi Kuvaa Wigi Kwenye Nembo Ya Taifa


Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM), ameiomba Serikali ipige marufuku matumizi ya nembo ya Taifa yenye picha ya ya mwanamke na mwanamume (Bibi na Bwana) kwa sababu mwanamke huyo amevaa wigi hivyo kutoakisi maisha ya Mtanzania.

Mbunge huyo ameomba mwongozo wa Spika leo Ijumaa Aprili 6, kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ambapo amedai katika nembo hiyo kuna bwana amevaa lubega ambaye anaakisi maisha ya Mtanzania.

“Bibi aliyevaa wigi haakisi maisha halisi ya Mtanzania hivyo naiomba Serikali isitishe matumizi ya nembo hiyo na izuie isitumike hadi ifanyiwe marekebisho kwani bibi amevaa wigi ambalo haliakisi maisha ya Mtanzania,” amesema Mlinga.

Akijibu mwongozo huo Chenge alihoji iwapo tukio hilo limetokea leo hadi Mbunge huyo anauliza.

“Narudi kwenye kanuni je, suala hili limetokea leo na kama halijatokea leo halipo kwenye kanuni,” amesema.

Amesema kwa sasa wanatakiwa kuheshimu sheria inayosimamia nembo

No comments:

Post a comment