Friday, 16 March 2018

Tanzania ya pili katika nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi Afrika

Jarida maarufu la Business Chief limeitaja Tanzania kama taifa la pili lenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Africa. Tanzania uchumi wake unakua kwa asilimia 7 imeshika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Cost ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia 8.5.

Orodha hiyo inayotangazwa kila mwaka, imesheheni mataifa ya Africa mashariki kwani ndio ukanda ambao umetajwa kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi, huku kilimo, utalii, usafiri, mawasiliano na biashara zikitajwa kama sekta zinazotazamwa na kuingiza vipato vikubwa.

Ukiondoa Tanzania na Ivory Coast mataifa mengine yaliyotajwa ni kama ifuatayo;

Senegal, Djibout, Rwanda, Kenya, Mozambique, Central African Republic, Sierra Leone Pamoja na Uganda.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: