Tuesday, 27 March 2018

Rayvanny aeleza ‘ubabe’ wa Diamond ndani ya WCB

Msanii Rayvanny kutoka WCB amesema katika utendaji kazi wake na Diamond ndani ya label hiyo hawajawahi kufikia hatua ya kupishana kauli katika kazi.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Makulusa’ ameiambia Funiko Base ya Radio Five mara nyingi mambo yanayotokea ni ya kawaida ingawa kuna mengine huonyesha kutopendezwa nayo.
“Nikikosea lazima anikoromee lakini kunikoromea hajawahi kwa sababu yeye siyo mtu wa kufokafoka lakini kitu akikukataza unajua hiki kitu hajakipenda, kwa hiyo unajua wewe hapo inabidi ujiongeze,” amesema Rayvanny.
Rayvanny na Diamond wameshafanya ngoma pamoja inayokwenda kwa jina la Salome, pia wamekutana katika ngoma ‘Zilipendwa’ ambayo iliwakutanisha wasanii wote walio chini ya WCB.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: