Wednesday, 21 March 2018

Label ya Young Dee yaandika barua ya wazi baada ‘Bongo Bahati Mbaya’ kufungiwa na Basata

Label ya King Cash ambayo inafanya kazi na rapa, Young Dee imeandika barua ya wazi kwa Baraza la Sanaa Taifa BASATA baada ya wimbo ‘Bongo Bahati Mbaya’ wa msanii wao huyo kufungiwe kwa kigezo cha kukosa uzalendo.
Uongozi wa label hiyo umetoa taarifa hii
Kama mwekezaji kupitia tasnia ya muziki wa Bongo Bleva napenda kufikisha kilio hiki kwenu BASATA kwa sababu pale muziki wa msanii wa King Cash unapofungiwa inamaanisha biashara ya King Cash imefungiwa, Hii inamaanisha nini? kama ikifungiwa miziki zaidi ya 100 kuna familia nyingi zitaathirika kupitia mnyororo huo.
Ukiangalia upande wa biashara ya King Cash, kampuni ya kitanzania inayoongeza ajira, kwa kujiari na kuajiri wengi zaidi ili kuunga mkono sera ya serikali ya ‘hapa kazi tuu’ baada yake mnaona kama ni kitu kidogo cha kukosoa tu kwa juu juu na kufungia bila kuangalia ni ubunifu wa namna gani ulitumika katika utunzi wa nyimbo ya moja ya msanii, tena mmefungia kwa kigezo cha wimbo haiendani na uzalendo, kweli jamani tutafika kwa namna hii.
Kama hamjui kila nyimbo tunayotoa ina bajeti yake ya kuizalisha na kuitangaza, na matarajio ya kipato kitakacho zalishwa na nyimbo hiyo ambapo faida itatutumika kuendesha maisha ya msanii na kutengeneza nyimbo nyingine. Sasa mnapo fungia nyimbo zetu inamaana tuache hii kazi ya muziki na familia zetu ziishi vipi?, kingine hebu tujifunze kupitia nchi jirani tunaweza kuwa na busara katika hili na ushirikiano ni jambo katika kukuza ustawi wa sanaa zetu.
Asante sana.
King Cash
Dar es salaam.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: