Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeimarisha ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kudhibiti umati wa watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao wamekusanyika nje ya mahakama, wasiingie kusikiliza kesi inayowakabili mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano.

Mbowe na wenzake wameshafikishwa mahakamani hapo wakitokea mahabusu ya Segerea wakikabiliwa na mashtaka manane yakiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline, Februari 16, mwaka huu, uasi na kuhamasisha chuki.

Wabunge wa Chadema, wafuasi na wananchi wengine wakiwa mahakamani kufuatilia kesi hiyo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: