Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema ipo haja ya yeye kuzungumza katika kikao kijacho cha Bunge juu ya hoja binafsi iliyowasilishwa na Mbunge mwenzake Hussein Bashe siku ya Jana (Machi 5, 2018).
Lema ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake maalumu baada ya kupita siku moja tokea Mbunge Bashe kupelekea barua hiyo kwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka iundwe kamati Teule ya kuchunguza baadhi ya mambo yanayoendelea katika ardhi ya Tanzania.
"Nina fikiri ninapaswa kusema kidogo juu ya hoja binafsi ya Mhe. Husein Bashe katika mkutano wa Bunge unaokuja. Hivi ni kweli tunahitaji Kamati teule kuhusu utekaji na kufifia kwa demokrasia nchini. Ni maamuzi ya CCM katika mikutano yao ya ndani ya Bunge na nje ya Bunge kuhusu hali ya demokrasia na siasa nchini, ujenzi wa vyama vya siasa na mikutano imepigwa marufuku", amesema Lema.
Pamoja na hayo, Lema ameendelea kwa kusema "wakati mambo haya yanaendelea kutokea Bunge limekataa hata kulipa matibabu ya Mh Lissu. Hakuna Mbunge hata mmoja wa CCM akiwemo Husein Bashe aliyewahi kwenda kumjulia hali Mh Lissu Hospital, najiuliza ni kwa nini ?. Mambo haya yako wazi hayahitaji PHD kujua msimamo wa Wabunge wa CCM kuhusu haki, ukweli na nuru ya mabadiliko".
Aidha, Lema amedai endapo Wabunge kutoka chama tawala wakibadili mtazamo wao kuhusu nchi basi hata Bunge litakua imara ambapo ndio msingi wa serikali bora unaotokana na wabunge majasiri.
"Bashe unafikiri Kamati Teule inaweza kuwa na maana kwenye Bunge hili ? hotuba za wapinzani Bungeni zimeendelea kuwa 'sensored' ndani ya Bunge na haya ni maoni mbadala ya ushauri kwa serikali lakini siku zote mmekaa kimya. Tunahitaji umoja wenu kwa masilahi ya haki ndani ya Bunge kwenye mambo yote yanayorudisha heshima ya Wabunge, wingi wenu umekuwa hasara kwa nchi badala ya faraja", amesisitiza Lema.
Lema ameendelea kusisitiza 
"Tunapoona maigizo yanayotaka kupotosha haki yanazingatiwa hapa ndipo tunapatwa hasira na kuondoa nidhamu katika mahusiano yasiyo na tija na nchi, hata hivyo andiko hili sio ugomvi lakini pia limejengwa hasira na hali zetu kisiasa tunayopitia, sisi Wabunge wa upinzani karibu wote tuna kesi sehemu mbali mbali nchini mmoja wetu sasa ni mfungwa (Sugu)". 
Kwa upande mwingine, Mbunge Godbless Lema amesema wanapitia katika maumivu makali katika siasa wanazozifanya hivyo hawaitaji kuona sinema tena zikiendelea kutoka kwa miongoni mwa wabunge wenzao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: