Saturday, 31 March 2018

Kampuni ya Sola za Sunking Yatoa msaada kwenye Kituo cha Kulelea watoto Yatima Arusha

Meneja wa mafunzo wa Sunking ,Immaculate Shija (Kushoto)akikabidhi baadhi ya misaada walioutoa kwa mkurugenzi wa kituo cha Nice Orphance Center,Florida Christian baada ya kutembelea

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya sunking wakishusha misaada mbali mbali ikiwemo vyakula 
 
Hii ndio Misaada iliyotolewa na kampuni ya umeme wa sola (sunking )Kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nice Ophance Center  kilichopo Bwawani wilayani Arumeru kilometa 35 kutoka jijini Arusha 

Meneja wa Sunking ,Immaculate Shija akiongea katika hafla fupi kabla ya kukabidhi msaada waliouleta kwa kituo cha kulelea watoto yatima ambapo pamoja na msaada huo wafanyakazi wa kampuni hiyo walishiriki kula chakula pamoja na watoto wa kituo hicho 

KAMPUNI ya kusambaza Umeme wa Sola Majumbani ya Sunking  Mkoa wa Arusha imekabidhi msaada wa Tenki la kuhifadhia maji lenye ukubwa wa lita 3000,vyakula pamoja na mtambo wa umeme wa Sola kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nice Orphance Center kilichopo katika kijiji cha Bwawani wilaya ya Arumeru,mkoani Arusha.

Akikabidhi msaada huo wenye thamani ya sh,milioni 6,leo machi 31,meneja Mafunzo wa kampuni hiyo, Immaculate Shija amesema kuwa msaada huo ni sehemu  ya faida kidogo wanayoipata na kuamua kuirejesha kwa jamii ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika masuala ya maendeleoo ya kijamii  

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo hicho cha kulelea watoto yatima ,Florida  Christian amesema kuwa kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2006 na hadi sasa kinawatoto wapatao 44 na kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa majengo ya kuwatunzia watoto,fedha za kuwasomesha pamoja na mahitaji mengine ya watoto hao.

Kampuni ya Sunking ni moja kati ya kampuni zinazofanya vizuri katika kuyaangaza maisha kupitia umeme wa sola na imefanikiwa kufunga mitambo zaidi ya 50,000 katika vijiji vilivyoko katika mikoa 26 iliyoifikia hapa nchini.

No comments:

Post a comment