Tuesday, 6 March 2018

KALANGA MBUNGE"WANANCHI WANATESEKA KWA KUKATIWA MAJI"

Wilaya ya Monduli mkoani arusha inakabiliwa na changamoto ya kukatiwa maji kutokana na shirika la umeme Tanesco kuidai ofisi ya Raisi Tamisemi deni la Shilingi milioni 115.

Akizungumza Mbunge wa Jimbo la Monduli Julius Kalanga amesema kuwa maji yamekuwa ya shida katika wilaya hiyo baada ya Shirika la Umeme (TANESCO) kukata umeme kwenye chanzo cha maji Ngaramtoni kutokana na deni hilo la Shilingi Milion 115.

Mbunge huyo amesema wananchi hawahusiki na malipo hayo na kinachotakiwa kifanyike ni deni hilo kulipwa ili huduma hiyo irudishwe haraka iwezekanavyo na kuepusha kadhia zaidi kwa wananchi ya maji.

Amesema mpaka sasa ameshawasiliana na naibu waziri wa maji pamoja na katibu wa maji ili kumaliza tatizo hilo ambalo linaathiri wananchi pamoja na Tasisi za Elimu pamoja na Shule.

No comments:

Post a comment