Thursday, 22 March 2018

Haji Manara afunguka mazito kuhusu Aslay


Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara ameibuka na kumtabiria mambo makubwa msanii wa BongoFleva Aslay kuwa siku si nyingi yeye ndio atakuwa mfalme katika tasnia ya muziki nchini Tanzania kutokana na kipaji chake cha kuimba vizuri alichonacho.
Manara ametoa kauli hiyo leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa kijamii baada ya kupita siku takribani mbili tokea msanii huyo alivyoachia video ya wimbo wake mpya uliopewa jina la 'nibebe' ambao mpaka sasa umekuwa wimbo pendwa kutoka kwa baadhi ya watu.
"Nishawahi kuandika huko nyuma juu ya hiki kipaji maridhawa. Dogo anajua sana na ninaamini 'one day' atakuwa Mfalme kamili, nimshauri kitu kimoja tu kuwa apige na bit za kuchezeka kidogo. Si unajua wabongo wanapenda mabuno. BASATA 'please' jamani hii nayo itakula umeme ?", amesema Manara.
Kama hujapata bahati ya kuitazama video mpya ya nibebe kutoka kwa Aslay Isihaka basi itazame hapa chini

No comments:

Post a Comment