Mkoani manyara wilaya ya Hanang, mbunge wa jimbo la hanang mhe,Dkt Mary Nagu hapo jana amekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya hiyo Bi. Sara Ally Msafiri kwa kile alichosema kuwa mbunge huyo amekuwa akifanya uchochezi wa kuichonganisha serikali na wananchi wake kuhusu utoaji michango ya elimu mashuleni wilayani humo.
Mkuu huyo wa wilaya amethibisha kumkamata mheshimiwa huyo leo asubuhi kwa tuhuma za uchochezi anazofanya hapo jimboni kwake.
“Ni kweli tumemkamata, tumemuweka ndani, anahamasisha wananchi kuhusu shughuli za maendeleo, anaongea kwenye mikutano kuwa DC anayoyafanya na sera zake hazina tija na anaagiza kwenye mikutano ya hadhara kwamba DC asifanye mikutano..”
amesema DC Bi. Sara alipokuwa akiongea na kituo cha Redio One katika kipindi kinachoruka asubuhi cha “Nipashe”.
Bi. Msafiri Ameendelea kusema kuwa mhe,Mary Nagu mbunge wa Hanang amekuwa akilalamika kwamba kuna kero mbalimbali katika wilaya yao na DC amekuwa hazifanyii kazi jambo ambalo DC Bi.Msafiri amelikana na kudai ni uongo kwani mheshimiwa huyo hajawahi kupeleka ofisini kwake kero yeyote ukizingatia wote wanakaa katika ofisi zilizo katika jengo moja.
“Kila anachokisema ni uongo,hajawahi kuleta kero yeyote ofisini kwangu,hajawahi kukaa kwenye vikao vyovyote na ni mjumbe vikao vya chama,tunakaa kwenye ofisi moja na hajawahi kuleta malalamiko yeyote yale lakini akiwa hapo nje ndiyo analalamikia kwenye mikutano.” Aliongezea Bi. Msafiri.
Aidha,Mkuu huyo wa wilaya amesema aliposikia habari hizo kwanza aliamua kumuacha afanye mikutano alipomaliza alimwandikia barua kumueleza juu tuhuma hizo na kumuelekeza asitishe mikutano mpaka pale watakapokaa pamoja kutafuta ufumbuzi suala hilo lakini hakuna majibu yeyote aliyorudishiwa jambo ambalo lilipelekea kuona mbunge huyo amekaidi amri kwani kesho yake Mhe. Nagu aliendelea kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mengine.
Mbunge Huyo ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za uchochezi na mpaka sasa hajaachiliwa. Kwa upande wake Bi. Sara Msafiri alipoulizwa ataachiwa lini..!! alisema bado wanaendelea kufanya kazi na wakijirishisha watamuachia.
“Tunaangalia tu,tunafanya kazi zetu na tukijiridhisha tunamuachia.” Alisema DC Bi. Msafiri.
Hii ni mara ya pili kwa mbunge huyo wa Hanang ambaye ni Kada wa CCM katika awamu hii ya uongozi wa Mhe. John Pombe Magufuli kushikiliwa kwa muda na jeshi la polisi.
Mwaka jana July 18 alishikiliwa na jeshi la polisi baada ya kutokea vurugu katika kikao cha kamati ya siasa ya chama hicho na kuachiwa baada ya kuhojiwa.
Dk Nagu amewahi kuwa waziri katika wizara kadhaa wakati wa utawala wa Serikali za awamu mbili zilizopita.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: