Monday, 5 March 2018

Bweni la Korogwe Girls lateketea kwa moto


MOTO umeteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe iliyoko mkoani Tanga na kuwaacha wanafunzi hao katika hali mbaya kufuatia mshtuko wa kupoteza vifaa vyao vyote.
Moto huo ulitokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo wakati wanafunzi takribani 40 wanaoishi katika bweni hilo wakiwa darasani wakijisomea.
Hata hivyo licha ya moto huo kutekeza bweni, hakuna madhara ya kimwili kwa upande wa wanafunzi hao isipokuwa kwa wale waliopata mshituko na kuzimia ambao wamelazwa katika Hospitali ya Magunga na Majengo wilayani humo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha moto kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.

No comments:

Post a comment