Tuesday, 20 February 2018

Wasichana wa shule na waalimu wanusurika kutekwa


Wanafunzi wa kike na waalimu wao huko kasikazini mashariki mwa nchi ya Nigeria wamripotiwa kufanikiwa kutoroka na kukwepa shambulio lililopangwa kufanyika katika shule hiyo na kundi la kigaidi la Boko Haram.

Taarifa kutoka nchini humo  inasema wanamgambo wa Boko Haram wakiwa katika gari dogo la mizigo waliwasili katika mji wa Dapchi, katika jimbo la Yobe siku ya Jumatatu jioni wakipiga risasi na kutega mabomu baada ya kusikika kwa kelele hizo wanafunzi hao walifanikiwa kutoroka.

Wakazi na wanamgambo wa kiraia wamesema kwamba kundi hilo la Kijihad walipanga kuwateka wanafunzi  na baada ya kukuta wanafunzi hawapo, waasi hao walifanya uharibifu na kuiba katika jengo hilo.

Mwezi Aprili mwaka 2014, kundi hilo la kigaidi la Boko Haram lilifanikiwa kuwateka wasichana 270 kutoka katika shule ya bweni ya Chibok huko kasikazini mashariki mwa mji huo mdogo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: