Jeshi la polisi mkoani Dodoma limewaonya viongozi wa dini mkoani humo ambao wanatabia ya kufanya vitendo vilivyo kinyume na mafundisho ya dini huku likiwaomba wananchi wawafichue viongozi hao ambao wenye tabia hizo.
Tokeo la picha la gilles muroto
Kamanda Gilles Muroto
Hayo yamesemwa leo Februari 14, 2018 na kamanda wa polisi mkoani humo, Kamishna msaidizi Mwandamizi wa polisi, Gilles Muroto.
Kamanda Muroto amesema kuwa kutokana na kukua kwa utandawazi kumekuwa rahisi kwa sasa watu kutumia nafasi hiyo kupotosha umma huku wakijinadi kuwa ni viongozi wa dini.
Muroto amesema viongozi wa dini watakaobainika kufanya vitendo hivyo au vya aina yoyote ile ya udhalilishaji jeshi la polisi halitawavumilia.
Kwa upande mwingine Kamanda Muroto amewaagiza viongozi wa dini kuhakikisha maeneo yao wanayofanyia ibada kunakuwa na ulinzi wakutosha ili kuzuia matukio ya kiuhalifu kutokea.
Onyo hilo linakuja baada ya mwanzoni mwa mwezi Januari Kiongozi mmoja wa dini aliyejitambulisha kwa jina la Nabii Tito kuhubiri kinyume na maadili ya umambo yaliyo nje na dini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: