Monday, 26 February 2018

Shy-Rose Bhanji akanusha taarifa ya kupinga Utawala wa Rais Magufuli


ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Bhanji amekanusha taarifa iliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa anapinga utawala wa Rais Dkt. John  Magufuli.


Taarifa hiyo ilionekana imeandikwa kwenye akaunti yake rasmi ya Instagram lakini  amesema ilikuwa imedukuliwa na watu wasiojulikana ambao wali-post ujumbe huo wenye nia ya kumchonganisha na Rais.

“Account yangu ya Instagram ilikuwa hacked na watu wasiojulikana ambao walipost vitu ambavyo sihusiki navyo. Naomba radhi kwa Rais wangu JPM na wote waliokerwa na jambo hilo,” ameandika ShyRose.

No comments:

Post a comment