Thursday, 15 February 2018

Polepole- ‘Kuna Mbunge wa Chadema ameomba kuhamia CCM’


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha CCM, Humphrey Polepole amedai kuwa, kuna Mbunge mmoja wa upinzani anataka kuhamia kwenye chama hicho.
Polepole ameyasema hayo leo Februari 15, 2018 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.
Polepole amesema Mbunge huyo wa Chadema ambaye hakumtaja jina alimuomba ahamie CCM na kwamba ushahidi kuhusu tukio hilo anao.
Amesema alimkatalia Mbunge huyo na kumuweka wazi kwamba kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020 CCM italitwaa jimbo lake na hatorejea tena bungeni.
“Kuna Mbunge wa Chadema hapa Dar es salaam ameniomba ahamie CCM, nimemkatalia na kumwambia wazi kuwa mwaka 2020 CCM itashinda jimbo lake mapema na asitegemee kurudi bungeni,ushahidi wa kumkatalia ninao,”amesema Polepole.

No comments:

Post a Comment