Wednesday, 28 February 2018

Mh. Lema apewa ujumbe mzito na mke wake

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) kufungwa mke wake amemuambia kuwa maisha ya siasa yanaendelea kuwa magumu sana.
Lema amesema kuwa Mke wake amemueleza kuwa kazi yao kwasasa imekuwa ni kuzika, mahakamani, polisi, hospitali na magereza.
Baada ya Sugu kufungwa,Mke wangu aliniambia”Godbless maisha ya Siasa yanaendelea kuwa magumu sana,kazi yenu sasa imekuwa ni kuzika, mahakamani,Polisi,Hospital na magereza” Mkti anasemaje?Mpeni moyo sana,mnapaswa kuilazimisha furaha ili msipoteze Imani na matumaini.unarudi lini,” ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: