Friday, 23 February 2018

Mbunge Mnyika : Wanataka kuifuta CHADEMA


Naibu Katibu Kuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Mhe. John Mnyika amefunguka na kusema kuwa kuna kila dalili serikali kupitia kwa msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mtungi.
Mnyika akiongea na waandishi wa habari leo Februari 23, 2018 amesema kuwa kuna njama ambazo zinapangwa kuhakikisha kuwa chama hicho kinafutiwa usajili wake jambo ambalo Mnyika anasema jambo hilo hawataliweza. 
"Msajili wa vyama vya siasa anasukumwa , dhamira yao ni kutafuta mwanya wa kukifuta Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jambo hili hawaliwezi na kama wanafikiri wanauwezo wa kuifuta CHADEMA wajaribu kufanya hivyo. Wafahamu kwamba wakizuia mlango wa demokrasia, watu watafanya siasa kwa njia nyingine, sisi tutakabiliana na msajili kwa njia yoyote kuhakikisha jambo hili halifanikiwi" alisema Mnyika 
Aidha Mnyika amesema kuwa Msajili wa vyama vya siasa nchini amekitaka chama cha Demokrasia na Maendeleo kujieleza kutokana na matukio ya Februari 16, 2018 hivyo amedai tayari wameshamjibu msajili huyo wa vyama vya siasa.
Mbali na hilo Mnyika amewataka wanachama wa CHADEMA pamoja na viongozi wake wakiwepo madiwani pamoja na wabunge wajilinde sana katika kipindi hiki kwani amedai kwa sasa wanashambuliwa kila kona kwa njia mbalimbali. 

No comments:

Post a comment