Wednesday, 21 February 2018

Madiwani wawili wa Chadema Arusha Mjini wahamia Ccm


Madiwani wawili  wa Chadema, katika Jiji la Arusha   wametangaza kujiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ( CCM).

Diwani wa kata ya Daraja Mbili Ndg. Prosper Msofe na Diwani wa kata ya Terrat Ndg.Obeid Meng’oriki (Chadema) wamejiuzulu uanachama na udiwani leo hii na kutangaza kujiunga na ccm kwa kile walichoeleza kuwa wamefanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Mh Rais Magufuli.

No comments:

Post a comment